Mchezaji wa timu ya Eastern Flames, Enekia Kasonga akiwa na mpira wake aliokabidhiwa baada ya kufunga hat-trick kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake nchini Saudi Arabia dhidi ya Al Riyadh.
Kwenye mchezo huo Enekia ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa Tanzania kwa wanawake alifunga mabao manne na kuisaidia Flames kupata ushindi wao wa kwanza tangu kuanza kwa msimu huu, hadi dakika ya mwisho ubao ulikuwa ikisoma 6-1.
Mechi ya kwanza Flames ilicheza dhidi ya Al Ittihad na kupokea kichapo cha mabao 3-0.
Huu unakuwa ni muendelezo wa Enekia kufanya vizuri tangu aanze kucheza soka la kulipwa ambapo kabla ya Saudia, aliwahi kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Morocco katika msimu wake wa kwanza akifunga mabao 27.