Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtanzania alamba dili CAF

Ameddd.jpeg Mtanzania alamba dili CAF

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtanzania Alfred Henry Amede ni miongoni mwa madaktari 44 kutoka nchi tofauti barani Afrika walioteuliwa kushiriki kozi ya siku mbili ya upambanaji na uzuiaji dawa zisizoruhusiwa michezoni itakayoanza kesho huko Johannesburg, Afrika.

Kozi hiyo ni maalum kwa ajili ya kujenga uwezo kwa watalaam wa tiba za michezo juu ya kupambana na kuzuia dawa zisizoruhusiwa michezoni pamoja na kutafuta timu ya watalaam watakaoshiriki katika udhibiti na vipimo vya dawa hizo kwenye fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Ivory Coast mwakani.

Mkuu wa kitengo cha udhibiti wa dawa zisizoruhusiwa michezoni cha Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Alexis Weber, Meneja wa kitengo cha kupambana na dawa zisizoruhusiwa michezoni wa Shikirisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Sherif Abou El Enein na mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya CAF, Raul Chipenda.

Akizungumzia uteuzi huo, Dk. Amede amesema amefurahishwa nao kwani unaenda kumpa maarifa zaidi juu ya namna ya kudhibiti dawa za kusisimua misuli.

"Ni semina elekezi kwa madaktari wa CAF. Inahusu 'Antidoping' (uzuiaji dawa zisizoruhusiwa michezoni) na namna ya kuhama kuingia kwenye nyaraka zisizotumia makaratasi.

"Lingine ndio hilo la maandalizi ya AFCON 2023," amesema Amede.

Amede ambaye ni daktari wa timu ya Singida Fountain Gate, amewahi kuhudumu katika timu tofauti za taifa za Tanzania lakini pia ni Mtumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa, Dodoma, Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live