Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtanzania afunguka alivyoandika rekodi kucheza na Messi

Kamungo Messiii.png Mtanzania afunguka alivyoandika rekodi kucheza na Messi

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Tanzania anayekipiga Ligi Kuu ya Marekani (MLS), Bernard Kamungo amesema ilikuwa tukio kubwa kwake kucheza kiwanja kimoja na staa wa Argentina, Lionel Messi.

Kamungo anayekipiga FC Dallas katika ligi hiyo amesema hilo ni tukio kubwa na kusema litabakia katika kumbukumbu zake kisoka.

Staa huyo alisema hayo mara baada ya kukutana na Msemaji wa Yanga, Haji Manara (ambaye yupo Marekani) jana na kukabidhiwa jezi ya Mabingwa wa Tanzania, Yanga SC. Zawadi ya jezi hiyo amekabidhiwa kama zawadi kwa Kaka yake nyota huyo ambaye ni shabiki wa Yanga.

“Ilikuwa fahari kubwa kuona nacheza kiwanja kimoja na staa wa dunia na kufunga bao pia. Hii ni kumbukumbu kubwa kwangu, licha ya kupoteza pambano lile dhidi yao.

"Baada ya mchezo ule katika chumba cha kubadilishia nguo hakukuwa na furaha kubwa, maana tulikuwa tumepoteza ile mechi,“ alisema Kamungo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live