Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtambo wa kumwaga maji Yanga kuongezewa kandarasi

Jesus Moloko Ducapel Jesus Moloko

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huenda mabosi wa Yanga wakamuongezea dili jingine mzee wa kumwaga maji ndani ya kikosi hicho Jesus Moloko.

Nyota huyo mkataba wake unatarajia kugota ukingoni mwishoni mwa msimu huu hivyo kama hataongezewa anaweza kujiunga na timu nyingine bure.

Moloko ni namba moja kwa kutengeneza pasi za mwisho ndani ya Yanga msimu wa 2022/23 akiwa ametoa jumla ya pasi tatu.

Yanga imefunga mabao 25 baada ya kucheza mechi 14 ni namba moja kwenye msimamo wa ligi inafuatiwa na Azam FC ambayo ina pointi 35 ikiwa imecheza mechi 15.

Mchezo ujao kwa Yanga ni dhidi ya Namungo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majaliwa, Desemba 7, 2022.

Nasreddine Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga hivi karibuni aliweka wazi kuwa kila mchezaji ndani ya kikosi ana umuhimu wake.

“Kila mchezaji kwenye kikosi ana umuhimu hivyo akikosekana mmoja huwa kunakuwa na shida kidogo licha ya kwamba lazima kila mmoja atimize majukumu yake,” amesema Nabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live