Simba ipo kwenye mazungumzo ya mwisho kumalizana na mshambuliaji Pa Omar Jobe kutoka Gambia. Mwanaspoti linafahamu
Simba itamtambulisha Jobe wakati wowote Leo mchana akija maalum kwa kazi ya kuimarisha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kufuatia mahitaji ya kocha Abdelhak Benchikha.
Klabu ya mwisho Jobe kuitumikia ni Zheniz ya Kazakhstan ukiwa ni usajili wa pili kwa Simba kwenye dirisha dogo la usajili akitanguliwa na kiungo Babacar Sarr raia wa Senegal.
Kutua kwa Jobe Simba inapiga karata ngumu kwani ripoti ya kocha Benchikha imetaka kuachwa kwa mshambuliaji mmoja wa kigeni kati ya wawili waliopo kwenye kikosi hicho.
Inaelezwa kwamba mshambuliaji Mzambia Mosses Phiri anapewa nafasi kubwa ya kuondolewa kwenye usajili kupisha nafasi ya Jobe aliyezaliwa miaka 25 iliyopita.
Simba inatakiwa kukata wachezaji wawili kupisha usajili wa wachezaji hao wawili wa kigeni ili wakidhi kanuni ya mahitaji ya wachezaji 12 wa kigeni.