Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msuva awapa masharti mazito Wydad Casablanca kumlipa bilioni 1.6

Msuva Simon Bilionea Simon Msuva

Thu, 14 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuwagaragaza mbele ya Kamati za Shirikisho la Soka Duniani, Mshambuliaji wa Tanzania Simon Msuva amepanga kupokea pesa zake kwa awamu moja tu na si vinginevyo kutoka katika klabu yake ya awali ya Wydad Casablanca.

FIFA imeiamuru klabu ya Wydad Casablanca kumlipa mchezaji huyo Tsh bilioni 1.6 ambayo kwa mujibu wa Msuva pesa hiyo inatakiwa kulipwa ndani ya siku 45 kutoka siku ya maamuzi ya FIFA.

Sasa Msuva amesema pesa hiyo hataki ilipwe kwa awamu bali yeye anataka kuipokea kwa mara moja tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live