Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msuva avunja ukimya Yanga

Msuva Visa Msuva avunja ukimya Yanga

Fri, 9 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva anayecheza soka la kulipwa Saudi Arabia akiwa na Al-Qadsiah, ametoa baraka zake kwa mfungaji bora wa Kombe la Shirikisho Afrika, Fiston Mayele kumaliza ukame wa miaka sita kwa Yanga kushindwa kutoa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara.

Msuva mwenye miaka 29 ndiye mchezaji wa mwisho kwa Yanga kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara, alifanya hivyo msimu miwili mfululizo 2014/15 na 2015/16 kabla kwenda Morocco kucheza soka la kulipwa.

Nyota huyo wa zamani wa Wydad Casablanca ya Morocco, anaamini kuwa Mayele ni kati ya washambuliaji bora Afrika hivyo yupo na ubora wa kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara licha ya kuwa na upinzani kutoka na Saidi Ntibazonkiza.

"Nadhani hata msimu uliopita alikuwa na nafasi hiyo ila bahati haikuwa upande wake, ni mchezaji mzuri na mwenye uwezo wa kufunga, uwepo wake na wachezaji wengine wa kigeni ambao wanafanya vizuri wanaamsha ari kwa wazawa," alisema Msuva na kuongeza;

"Yupo na nafasi ya kuwa mfungaji bora japo mchezo mmoja unaweza kubadili mambo, nikiri pia navutiwa sana na uchezaje wake."

Ndani ya msimu wake wa mwisho Yanga, Msuva alimaliza kama kinara wa mabao wa Ligi Kuu akitupia 14 akilingana na Abdulrahman wa Ruvu Shooting na wote kupewa tuzo, ikiwa ni msimu wa tatu mfululizo kwa Yanga kubeba kiatu baada ya Msuva na Amissi Tambwe kufanya kweli.

Mshambuliaji huyo alikuwa sehemu ya safu kali ya ushambuliaji ya Yanga ambayo pia ilikuwa na nyota wengine ambao walikuwa kwenye ubora wao kama vile Chirwa, Amis Tambwe na Donald Ngoma ambao pamoja na wengine wameifanya Yanga ipate ubingwa msimu huo kwa tofauti ya mabao licha ya kulingana pointi na wekundu wa Msimbazi Simba.

Yanga ilimaliza ligi ikiwa na mabao 43 ambayo ni tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa wakati Simba ikiwa na mabao 33 kama tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa, na hivyo kuipiku Simba kwa jumla ya mabao 10 ya kufunga.

Chanzo: Mwanaspoti