Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msuva atoa somo zito kwa wanasoka, ukata wamuhamisha Mji

Msu Talk Simon Msuva

Thu, 14 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva ametoa somo zito kwa wachezaji wa Kitanzania walio na ndoto za kucheza kandanda nje ya mipaka ya Tanzania.

Msuva ameeleza kuwa mambo si rahisi kama wengi wanavyodhani bali kuna changamoto mbali mbali watakazoweza kukutana nazo katika vilabu tofauti licha ya ukubwa wa majina ya vilabu hivyo.

Kuna ujanja ujanja mwingi ambao kwa vyovyote hutarajii kukutana nao kwa sababu ya ukubwa wa Vilabu vyao, kitu ambacho kinaweza kukukatisha tamaa kama mtafutaji.

Msuva ameyaeleza hayo leo Julai 14, wakati akieleza kwa undani sakata lake lililomfanya kuishitaki klabu ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco mbele ya Shirikisho la Soka Duniani, FIFA.

Msuva ameeleza kuwa kabla ya kuamua kuondoka Wydad Casablanca amekutana na changamoto nyingi sana zilizokuwa zinafanyika nje ya makubaliano ya kimkataba.

Katika melezo yake msuva ameeleza kufikia hatua ya kutolipwa mishahara na kushindwa kulipa kodi hivyo akahama mji wa Casablanca na kuhamia Jaddida kwa rafiki kwa sababu hakua na uwezo wa kujilipia baadhi ya huduma.

"Kocha aliona kiwango changu kikiporomoka aliponiuliza akagundua changamoto kadha wa kadha zinazonikabili hivyo akawa ananipa fedha kunisaidia nisiache kuja mazoezini na niweze kujihudumia katika baadhi ya viyu, lakini aliniambia suala la mkataba yeye halimuhusu"

Msuva pia ameeleza mchezo mchafu aliokuwa akifanmyiwa na Rais wa klabu ya Wydad ambae alikuwa akimpigia simu kumuelezea matatizo yake na kumuita nyumbani, lakini anapofika nyumbani anakuta Rais huyo ameacha maagizo kwa walinzi wamueleze Msuva kuwa hayupo.

Matokeo ya kesi hiyo FIFA wameiagiza Klabu ya Wydad Casablanca kumlipa Msuva kiasi cha Tsh Bilioni 1.6 na zitalipwa ndani ya siku 45, lakin pia Wydad wana nafasi ya kukata rufaa ndani ya siku 10 tangu hukumu ilipotoka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live