Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msuva ashushiwa Wareno Algeria

Wareno Algeria Msuva ashushiwa Wareno Algeria

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji Mtanzania Simon Msuva atakaporejea klabuni kwake JS Kabylie tu atakutana na benchi jipya la ufundi chini ya kocha Mreno Rui Almeida.

Almeida ametangazwa kuwa kocha mpya wa Kabylie akichukua mikoba ya kocha mzawa Youcef Bouzid ambaye alitangaza kuachana na klabu hiyo mwezi uliopita.

Almeida (54) ametua na wasaidizi wake wawili wakiwemo kocha msaidizi Pedro Miguel Mimoso na kocha wa mazoezi ya viungo Sergio Mauricio Querido.

Msuva ambaye yupo nchini Saudi Arabia na kikosi cha Taifa Stars kilicholazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Sudan atakutana na makocha hao ambao wameshaanza kazi leo.

Habari njema kwa Msuva ni kwamba Almeida anapenda kutumia mfumo wa 3-5-2 ambao mshambuliaji huyo amekuwa akikutana nao klabu zake mbili zilizopita za Wydad Athletic ya Morocco na Al Al Qadsiah FC ya Saudi Arabia.

Msuva tangu atue JS Kabylie ikiwa chini ya Bouzid aliyekuwa anatumia mfumo wa 4-3-3 hakuwa na mwanzo mzuri ndani ya klabu hiyo iliyomsajili miezi michache iliyopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live