Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msuva apumzishwa Dar

Msuva+pic Msuva apumzishwa Dar

Fri, 2 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva ambaye bado yupo nchini amepewa mapumziko mafupi na viongozi wa klabu yake ya Wydad Casablanca baada ya kutekeleza majumu ya kitaifa hivyo anaweza asiwe sehemu ya mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chief ya Afrika Kusini.

Wydad Casablanca tayari wamejikatia tiketi ya kucheza hatua ya robo fainali kufuatia kufanya kwao vizuri kwenye michezo minne iliyopita huku wakivuna pointi 10 baada ya kuzifunga Kaizer Chief, Petro Atletico na Horoya kwenye mchezo wa kwanza halafu kwenye mchezo wa marudiano wakatoka nao suluhu.

Msuva ataendelea kuwapo nchini kwa mapumziko hayo mafupi hadi Jumamosi, Aprili 3 ambapo atatakiwa kuanza safari ya kurudi Morocco, “Naona viongozi watakuwa waliona kuna umuhimu wa pengine kunipa muda wa hata kusalimiana na ndugu zangu maana kuna kipindi huwa nashindwa hata kufika nyumbani, baada ya mechi huwa nageuza.”

“Kazi kwa kiasi kikubwa tumeifanya mapema na ndio kitu ambacho tulikuwa tukikitaka ili tuwe na muda wa kupumua kabla ya kutumia tena nguvu kubwa kwenye michezo ya mtoano (robo), naamini tunaweza kutwaa ubingwa wa Afrika,” alisema.

Jumapili ya wiki iliyopita, Msuva alitupia bao kwa Taifa Stars ambayo ilikuwa ikikamilisha ratiba dhidi ya Libya kwenye kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za Afcon ambazo zinatajiwa kufanyikwa mwakani nchini Cameroon.

Msuva aliongeza kwa kusema, “Yeyote ambaye tutapangwa naye kwenye hatua inayofuata naona sawa tu kwa sababu haya ni mashindano na huwezi kukwepa kukabiliana na timu bora na ili utwae ubingwa lazima uzishinde timu za namna hiyo.”

Related Aussems, Migne waiteta Simba



Atapigwa mtu nyingi
Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz