Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msuva apiga hesabu kali

MSUVA 003?fit=700%2C457&ssl=1 Simon Msuva

Mon, 24 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva ambaye anaichezea Al-Qadsiah amesema anaamini kuwa msimu ujao wa soka huko Saudi Arabia unaweza kuwa na neema zaidi kwake kuliko huu unaomalizika.

Msuva ambaye huu ni msimu wake wa kwanza kucheza soka la kulipwa nchini humo, amejikuta na chama lake wakiwa kwenye mapambano ya kuhakikisha wanasalia kwenye ligi hiyo badala ya kuwa kwenye vita ya kupanda ligi kuu.

Nyota huyo wa zamani wa Wydad Casablanca na Difaa El Jadida za Morocco alisema idadi kubwa ya wachezaji ambao wameingia kwa wakati mmoja kwenye kikosi hicho pengine ni sababu ambayo imechangia.

"Tunaweza kubakia kwenye ligi, tupo nafasi moja juu ya hatari ya kushuka daraja, Jumatano tutacheza na maandalizi ya mchezo yapo sawa, ligi ni ngumu sana na kila mmoja wetu hasa ambao ni wageni tumekuwa tukihakikisha tunaizoea na kucheza kwenye viwango vyetu," alisema.

Aliongeza kwa kusema,"Natamani kwenye uchezaji wangu soka hapa nicheze ligi kuu, najua hilo linawezekana, timu yetu ni nzuri, inaweza kupandambana na kupanda daraja, ni suala la muda, kilichotokea msimu huu haikuwa matarajio yetu lakini tutapambana na kujaribu tena bahati yetu msimu ujao."

Katika Ligi hiyo ya daraja la Kwanza Saudi Arabia, Msuva licha ya ugeni wake ameweka kambani mabao manane na anatarajiwa tena, Jumatano kuongoza mashambulizi ya timu hiyo dhidi ya Al Qaisumah wakiwa ugenini.

Al-Qadsiah anayoichezea Msuva ipo nafasi ya 15 wakiwa na pointi 28 kwenye msimamo wa ligi hiyo huku wakipishana mabao tu na Najran ambao wapo kwenye mstari wa kushuka daraja

Chanzo: Mwanaspoti