Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msuva aibukia KenGold

Msuva Family James Msuva na Simon Msuva.

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya KenGold imemsajili winga wa KMC, James Msuva, kwa ajili ya kuichezea timu hiyo Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Taarifa iliyotolewa jana na klabu hiyo, imesema Msuva ni mmoja wa wachezaji watakaoichezea timu hiyo, itakayocheza kwa mara ya kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kupanda msimu huu.

Msuva, ambaye ni mdogo wa winga wa timu ya taifa ya Tanzania, Simon Msuva. Mbali na kuichezea klabu ya KMC, amewahi pia kuichezea klabu ya Mbao FC.

"Nina furaha kuwa sehemu ya familia ya KenGold, kila timu inayoingia kwenye Ligi Kuu inakuwa na malengo yake, na sisi pia tunayo ya kwetu, lakini makubwa ni ya klabu kuona inafanya vyema na inabaki kwenye ligi ikiwa kwenye nafasi nzuri, naamini kwa kikosi kilichopo na mazoezi tunayofanya tutafanya kitu ambacho wengi hawawezi kutarajia kwa sababu ni timu iliyosheheni vijana wengi wenye ari na vipaji," alisema Msuva.

Mbali na hilo, klabu hiyo pia imefanikiwa kumsajili mshambuliaji wa   wa TMA Stars, Ramadhan Chobwedo, ambaye alikuwa mmoja wa waliofunga mabao mengi kwenye Ligi ya 'Championship' msimu uliomalizika.

KenGold imeshinda vita ya kumuwania mshambuliaji huyo aliyekuwa akitakiwa kwa udi na uvumba na Prisons.

"Nimefurahi sana kwa kusajiliwa na KenGold. Nipo hapa kuitetea nembo ya klabu hii, na ninawaahidi mashabiki wa timu kuwa tutapambana sana, japo ni wageni kwenye ligi lakini lengo letu ikiwezekana ni kuchukua moja kati ya nafasi nne za juu, na ikishindikana kabisa basi tubaki kwenye ligi tukiwa kwenye nafasi nzuri," alisema mshambuliaji huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: