Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msuva aibukia Cambiasso dhidi ya Simba

Msuva Vs Simba Msuva aibukia Cambiasso dhidi ya Simba

Tue, 15 Mar 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Straika Simon Msuva ni kati ya wachezaji wa Cambiasso ambao wanacheza mechi ya kirafiki leo Machi 15 dhidi ya Simba, Uwanja wa Mo Simba  Arena, uliopo Bunju.

Msuva yupo nje ya timu yake ya Wydad ya Morocco, huku sababu ikitajwa na kudai maslahi yake na kukaa kwake Cambiasso ni kulinda kiwango chake.

Msuva anajituma kama vile ni mchezo wa kuvuna pointi tatu, huku akionekana ana usongo wa kucheka na nyavu.

Mshambuliaji huyo mwenye uwezo mkubwa wa kufunga amedhihirisha hilo baada ya kutumia dakika 10 za kwanza katika mchezo huo kuwaanfdikia Cambiasso bao la uongozi.

Msuva alifunga bao ndani ya 18, huku akimuacha Kakolanya hana la kufanya zaidi ya kuokota mpira nyavuni.

Simba ilipata bao la kusawazisha kupitia kwa mchezaji wao kiraka Erasto Nyoni baada ya kupokea kona aliyopiga Clatous Chama.

Kwa ujumla mechi ilikuwa 50 kwa 50, ingawa Simba imeonekana kucheza kimbuni zaidi kipindi cha kwanza.

Kiungo wa Simba, Clatous Chama alipata nafasi ya kufunga baadaya kumtoka beki wa Cambiasso lakini shuti lake halikuwa na matunda lilishia kugonga mwamba na mpira huo ulirudi ukakutana na Chris Mugalu ambaye alipaisha.

Mchezo ni mapuziko Simba 1-1 Cambiasso.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz