Nyota mpya wa Al-Najma ya Saudia, Simon Msuva ameamua kugeukia upande wa biashara ya nguo kwa kuja na chapa ya ‘Air Msuva’ ikiwa ni sehemu ya ubunifu kutokana na staili yake ya ushangiliaji ‘sarakasi’ ambayo aliionyesha kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika, Ivory Coast.
Msuva ambaye alifunga bao pekee la Tanzania kwenye fainali hizo, alikuwa kivutio kwa sarakati aliyoruka baada ya kuitanguliza Taifa Stars wakati wa mchezo wa makundi dhidi ya Zambia, mechi hiyo iliisha kwa sare ya bao 1-1.
Ukurasa rasmi wa Caf ni miongoni mwa mitandao ya kijamii ambayo ilimposti Msuva na kuandika umepiga hapo, hivyo nyota baada ya fainali hizo, nyota huyo akaona atumia fursa hiyo kwa kuja na bishara yake.
“Naomba Watanzania wanisapoti kwenye hili, mimi ni kijana wao. Hii ni kwa yeyote ambaye anapenda na kuthamini ninacho kifanya,” alisema Msuva.
Kupitia chapa ya Air Msuva, nyota huyo wa kimataifa wa Tanzania ameingia rasmi kwenye soka la bishara ya nguo kwa kuuza, masweta ‘prova’, t-shert na singlendi zenye picha ya shangilia ya bao lake dhidi ya Zambia.