Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msuva aanika ukweli kutua Yanga

Msuva 8145960 Simon Msuva

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuhusishwa kujiunga na Yanga, winga wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’, Saimon Msuva kwa mara ya kwanza tangu aachane na timu ya JS Kabylie ya Algeria amesema kuwa lolote linaweza kutokea akacheza ligi ya ndani au nje ya nchi.

Msuva ambaye aliachana na timu hiyo mwishoni mwa mwaka jana baada ya kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa kutoka kwake, kwa sasa yupo na Stars akijiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) 2023.

Mwanaspoti lilipomtafuta Msuva ili kuzungumzia mustakabali baada ya taarifa kuzagaa kuwa anatarajiwa kujiunga na Yanga, alijibu kuwa hakuna linaloshindikana kwenye soka.

“Nina ofa japo nyingine ni tetesi zinazungumzwa tu kutokana na kubaini mimi ni mchezaji huru. Ninachoweza kusema kwa sasa tusubiri mambo yakamilike kila mmoja atafahamu nitacheza wapi, lakini jambo la msingi ni kwamba chochote kinaweza kutokea,” alisema Msuva.

“Kucheza Tanzania au nje ya Tanzania lolote linawezekana tusubiri muda utazungumza. Sitaki kuwa mzungumzaji kwa sasa napambana kuhakikisha Taifa Stars inafanya vizuri kwenye fainali za Afcon 2023.”

Msuva alifanikiwa kuzitumikia timu kubwa ikiwemo Wydad Casablanca na Difaa El Jadida za nchini Morocco.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: