Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msuva Yanga ndo basi tena, arudi Saudia

Simon Msuva Saudia Simon Msuva

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa Kimataifa kutoka Tanzania, Simon Msuva ndio basi tena Yanga. Hii ni baada ya kutambulishwa Al Najmah inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza Saudi Arabia.

Kipindi cha dirisha dogo la usajili kulikuwa na tetesi za nyota huyo aliyewahi kutamba akiwa na Yanga, huenda akarejea kwenye timu hiyo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara akiwa mchezaji huru baada ya kuvunjiwa mkataba na JS Kabylie ya Algeria.

Wakati wengi wakiamini anarudi Jangwani alikioondoka tangu msimu wa 2017/18 na kutua Difaa El Jadida, msuva hakurejea kucheza Ligi Kuu Bara na ameendelea kucheza nje ya nchi ikiwa ni mara ya pili anarudi Saudi Arabia kucheza Ligi Daraja la Kwanza.

Baada ya utambulisho huo, kwenye akaunti ya klabu ya Instagram, Msuva aliongea akifurahia kujiunga na timu hiyo ambayo kwenye msimamo wa ligi hiyo, iko nafasi ya tisa baada ya kucheza michezo 18 na ina pointi 25.

"Nafurahia kusaini Al Najma, nafurahi kurudi Saudi Arabia na tutaonana baadaye,” alisema Msuva.

Msuva atajiunga na timu hiyo baada ya kumaliza mechi za Stars ambayo inacheza leo na DR Congo mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kwenye Fainali za Afcon zinazoendelea Ivory Coast.

Hii ni timu ya tano kwake kucheza nje ya nchi tangu alivyoondoka Yanga msimu wa 2017-18 na amepita Difaa El Jadida na Wydad Casablanca za Morocco, Al Qadsiah ya Saudi Arabia na JS Kabylie ya Algeria.

Kwenye Fainali za Afcon ameifungia bao moja Stars dhjidi ya Zambia na kufikisha mabao 22 tangu aanze kuichezea timu hiyo.

Chanzo: Mwanaspoti