Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msuva: Uzoefu utanisaidia Saudi Arabia

Msuva 3.jpeg Simon Msuva

Wed, 31 Jan 2024 Chanzo: Dar24

Kiungo Mshambuliaji ‘Winga’ Simon Msuva, ametamba kuwa uzoefu na juhudi aliouonesha katika timu alizocheza ndiyo sababu ya kupata timu nchini Saudi Arabia.

Nyota huyo wa timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ hivi karibuni alikamilisha usajili wa kujiunga na Al Najmah inayoshiriki Ligi daraja la Pili nchini Saudi Arabia akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na JS Kabylie ya Algeria.

Hii ni mara ya pili kwa Msuva kucheza soka la kulipwa nchini humo, ambapo mara ya kwanza aliitumikia Al-Qadsiah inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Hata hivyo, Msuva hakudumu sana Al-Qadsiah baada ya kucheza msimu mmoja kisha kuondoka na kujiunga na Kabylie ambayo hivi karibuni alivunja mkataba.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Msuva amesema anafurahi kuona kiwango chake kikizidi kupanda na kupata nafasi ya kuonwa na timu mbalimbali.

Msuva amesema pamoja na kupata timu Saudi Arabia, amejipanga kucheza nchini humo kwa muda mrefu kwa kuwa tayari ana uzoefu wa soka na mazingira.

Ameongeza kwa kuwataka wachezaji wenzake kuendelea kujituma, kukuza viwango vyao kwa lengo la kuzivutia timu nyingine na kwenda kucheza soka la kulipwa.

Chanzo: Dar24