Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msuva: Ni faida kuanza na mpinzani tunaemjua

Msuva Simon 1 1140x640 Simon Msuva

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Straika Saimon Msuva ambaye anaichezea JS Kabylie ya Algeria, alisema kuanza na mpinzani ambaye unamfahamu vizuri inaweza kuwa faida kwa Taifa Stars kwenye safari ya kwenda fainali za Kombe la Dunia.

“Kwanza kabisa nina furaha kuwa sehemu ya kikosi hiki. Tuna mchezo mgumu mbele yetu, lakini kama timu tunajiandaa kuhakikisha tunakuwa na mwanzo mzuri pamoja na kwamba tunaanzia ugenini, hilo siyo tatizo kabisa kwetu kwa sababu siku hizi mpira hauna cha nyumbani wala ugenini,” alisema Msuva.

“Tumecheza na Niger mara mbili nakumbuka kwenye mechi za kufuzu kwa Afcon. Wana timu nzuri japo, lakini maandalizi yetu yalitufanya kuwafunga nyumbani na kwao tulitoka sare. Muda umepita na wanaweza kuwa wamebadilika, hivyo tunatakiwa kuwa bora zaidi ili kuendelea kufanya vizuri dhidi yao.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live