Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msolla apigwa zengwe Uchaguzi bodi ya Ligi

Msollla Mshindo Mwenyekiti wa Yanga, Dkt. Mshindo Msolla

Sun, 31 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Dk Mshindo Mbette Msolla, ameenguliwa kwenye uchaguzi wa Bodi ya Ligi Tanzania kwa kile kilichoelezwa hajakidhi vigezo kanuni ya 9 (7) ya vigezo vya kanuni za uchaguzi za TFF toleo la 2021.

Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, Msolla ameenguliwa kwa kutowasilisha nakala halisi za vyeti vya Taaluma, wakati Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Ally Mangungu hakuhudhuria usaili.

Mwenyekiti wa sasa Bodi, Steven Jarvis Mnguto wa Coastal Union ndio mgombea pekee aliyeitishwa kwenye nafasi hiyo kuelekea uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 27, mwaka huu mkoani Kigoma, huku Mwenyekiti wa Azam FC, Nassor Idrisa ‘Father’ pekee akipitishwa kugombea nafasi ya Makamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live