UONGOZI wa klabu ya Yanga pamoja na wachezaji wa kikosi hiko, leo asubuhi wameungana na wananchi wa Tanzania katika kuaga mwili wa aliyekuwa rais wa Jamhuri ya Tanzania, John Magufuli katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Yanga walianzia katika uwanja wa Uhuru na baada ya hapo walitoka na moja kwa moja mpaka katika ofisi ya Mkoa CCM, Lumumba.
Mwanaspoti lilikuwa bega kwa bega likishuhudia nyota hao wakitia saini katika kitabu hiko kilichokuwa nje ya jengo hilo.
Wachezaji hao waliongozwa na Mwenyekiti wa klabu, Dk Mshindo Msolla, Mshauri wa Yanga, Senzo Mbatha , Msemaji wao Hassan Bumbuli na Mhamasishaji Antonio Nugaz.
Huku upande wa benchi la ufundi liliongozwa na kaimu kocha mkuu, Juma Mwambusi akiongozana na nyota wake.