Mwenyekiti wa Yanga anayemaliza muda wake, Dk Mshindo Msola amesema hakurudisha fomu yake ya kugombea nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu wa klabu hiyo unaotarajia kufanyika Julai 9, mwaka huu na kumuacha Injinia Hersi Said pekee.
Msola amedumu madarakani kwa miaka minne tangu achaguliwe na wanachama lakini sasa hatagombea kwa kile alichoeleza kuwa ni kupisha wengine kwani yeye jukumu lake kubwa amelitimiza.
“Nilisema tangu awali kuwa mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu ukikamilika basi sitakuwa mmoja wa wagombea, maana nimeufanya mchakato huo hatua ya awali ikiwemo mabadiliko ya Katiba". alisema Msolla na kuongeza,
“Ingawa mchakato huko mbele bado haujakamilika lakini najivunia kukamilisha Katiba mpya ambayo itakuwa ni muongozo wa kila kitu ndani ya klabu sina budi kukaa kando, tunafanya kazi kwa umoja”.