Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msitafute mchawi, tatizo la Simba liko hapa

Ngomaaaa WA0002 Msitafute mchawi, tatizo la Simba liko hapa

Sun, 26 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huu msimu wa tatu Sasa Simba SC imekua ikipitia wakati mgumu kwenye kiungo cha ukabaji, hapo nyuma walikua na Taddeo Lwanga & Jonas Mkude ambao walionekana angalau wanapaweka salama (Angalau).

Nyuma ya hapo walikua na James Kotei na Fraga, hawa walikua dawa kabisa, walinzi akina Wawa hata Aishi Manula walikula sana bata, fullbacks zilipanda zilivyotaka.

Msimu jana Zoran Maki aligundua shida hiyo kuna baadhi ya mechi akalazimisha kucheza na Augustine Okrah (just imagine). Simba hii Kanoute na Ngoma Box ya Ulinzi wanacheza ila wanaonekana kutamani zaidi box ya juu (Box to box).

Mnyama msimu jana amepata tabu sana hilo eneo kwa kumtumia Mzamiru na Kanoute, Msimu huu Niliamini nafasi ya kwanza kusajili ingekua kiungo wa ukabaji.

Akaletwa Fabrice Ngoma, Ni bonge la Mehezaji lakini Ngoma sio Namba 6, Ngoma ni Kanoute & Muzamir yani anacheza zaidi box ya juu ya chini ni dharula tu (Box to box).

Ngoma Akiwa Vita Club alikua anacheza Namba 8, 6 alikua Nelson Munganga (Captain), Akiwa na Raja Casablanca alicheza amba 8, 6 Zakaria Elward au Omar Arjun.

Ni Simba ndio wameona Ngoma ni Namba 6, Hawezi kukatakaa hiyo nafasi kwasababu ni Mchezaji lakini hawezi kupefrom kwenye daraja linalotakiwa.

Kabla ya yote mengine, Simba inatakiwa irudishe nguvu kwenye kiungo na msingi wa hilo ni kusajili Kiungo bora wa ukabaji ambaye anaweza kuwafanyia Uchafu wote wakiwa hawana mpira.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live