Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msimfananishe Pacome na Zidane - Saleh Jembe

Pacome Shows Msimfananishe Pacome na Zidane - Saleh Jembe

Fri, 25 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Legend kwenye masuala ya habari za michezo Bongo kitaifa na kimataifa, Saleh Ally Jembe amefungukia kuhusu uwezo wa nyota wa Yanga Pacome ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu Miguel Gamondi.

Nyota huyo wa Yanga ameaanza kupenya kikosi cha Yanga ambacho kinashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na ligi pia baada ya kuonyesha uwezo mkubwa na kufanikiwa kuifungia timu yake bao moja katika mabao 5-0 yaliyofungwa dhidi ya KMC juzi.

“Pacome ni mchezaji mzuri lakini tusimfafanishe na Zidane. Pacome ana uwezo anajiamini na ana uwezo wa kuibeba mechi, kwa sasa ameanza kuizoea ligi lakini ushabiki tuuache.

“Daraja la Zidane ni la Dunia ;lakini Pacome tunahitaji kumuona zaidi na zaidi kuona kile alivhonacho. Ninatamani kuona ushindani wa kile wanachokifanya akina Pacome na Ngoma, wazawa nao wafanye vile vile au zaidi ya vile," amesema Jembe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: