Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msimamo baada ya Ligi Kuu 2023/24 kumalizika, kila timu imevuna ilichopanda

Yanga Azam Matokeo Msimamo baada ya Ligi Kuu 2023/24 kumalizika, kila timu imevuna ilichopanda

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mechi nane za Ligi Kuu ya NBC zimepigwa kwenye viwanja vinane tofauti leo, Jumanne, Mei 28, 2024, ambazo zilikuwa mechi za mwisho za kufunga msimu wa mwaka 2023/24.

Yanga ambao tayari ni mabingwa wameendeleza ushindi kwa kuwafunga Tanzania Prisons na kufikisha alama 80, Azam FC wameshinda dhidi ya Geita na kufikisha alama 69 sawa na Simba ambao wameshinda dhidi ya JKT Tanzania na kufikisha alama 69 lakini Azam wana faida ya tofauti ya mabao mengi ya kufunga hivyo Simba wameshika nafasi ya tatu.

Kwa matokeo hayo, Yanga na Azam FC ndiyo wataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika msimu ujao huku Simba na Coastal Union ambao wamemaliza nafasi ya nne watashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Mtibwa ambaye ameshashuka daraja ataungana na Geita Gold ambaye naye ameshuka daraja moja kwa moja huku Tabora United na JKT Tanzania wakitakiwa kucheza playoff.

Mshindi wa playoff hiyo atabaki ligi kuu lakini atakayeshindwa atakwenda kucheza playoff na Biashara United ya Championship ili kusaka tiketi ya kucheza Ligi Kuu msimu ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live