Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msimamo Ligi Kuu NBC Machi 15

Msimamo NBC LIGI March Msimamo ulivyo wa Ligi Kuu Bara (NBC Primia Ligi) leo Machi 15

Tue, 15 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi Kuu Tanzania Bara(NBC Primia Ligi) 2021/2022 imeendelea leo kwa mchezo mmoja katika Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Wanajeshi wa Mpakani,Biashara United mambo yanazidi kuwanyookea baada ya leo kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Maafande wa Jeshi la Magereza Timu ya Tanzania Prisons.

Magoli ya Biashara katika mchezo wa leo yamefungwa na Deogratius Judika Mafie dakika za 26 na 34 huku la Prisons likifungwa na Ezekiah Mwashilindi dakika ya 68 ya mchezo.

Ushindi huo unawafanya Biashara kukamata nafasi ya 14 wakiwa na alama zao 19 baada ya michezo 18, Huku Tanzania Prisons jahazi likizidi kuzama wakiwa wanabruza mkia katika msimamo wa Ligi wakiwa na alama 13 baada ya michezo 18.

Yanga bado kinara akiwa kileleni na alama zake 45 baada ya kucheza michezo 17 akifuatiwa na Bingwa mtetezi Simba SC nafasi ya Pili wenye alama 37.

Tazama msimamo wa Ligi ulivyo leo Machi 15

Chanzo: www.tanzaniaweb.live