Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msimamizi wa Chasambi: Shaffih Dauda alitaka maslahi binafsi

Chasambi Msdf Ladack Chasambi.

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msimamizi na Mwanasheria wa mchezaji mpya wa Simba, Ladack Chasambi amesema kuwa kitendo cha Mchambuzi nguli wa masuala ya soka nchini, Shaffih Dauda kujitokeza kwenye vyombo vya habari na kudai kuwa alikuwa na ofa ya kumpeleka mchezaji huyo Ulaya ni uongo.

Msimamizi huyo wa Chasambi amesema kuwa jambo alilolifanya dauda ni kinyume na sheria na hata weredi wa masuala ya soka kwani hana haki ya kuzungumzia masuala ya mchezaji bila ridhaa yake na hata hivyo, ameshafungiwa kujihusisha na mazuala ya soka hivyo alichokifanya ni hiana kwa kijana huyo baada ya kujiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar.

“Shaffih alimtafuta Chasambi nakumuambia amemtafutia tim Ulaya, lakini Chasambi akamuambia zungumza na Meneja wangu na kweli alitututafuta.

“Tukamuambia kama kweli Ofa ipo mezani ailete lakini hakuna Ofa aliyoleta hivyo baada ya kuona kaenda Simba ndio kaamua kuongea haya ili kumchafua Mchezaji. Alitaka amsainishe kwenye academy yake kisha atengeneze mazingira ya kupiga pesa.

“Sisi tunaona haya yote yametokana na (personal interest) yeye kumkosa Chasambi kwenye Kampuni yake ndio maana ameongea haya yote. Lengo lake ilikuwa kutaka kumchafua mchezaji na klabu.

"Kama angekuwa na nia ya kumsaidia kweli angeleta ofa kwamba timu hii na hii zinamtaka Chasambi na dili lao ni pesa kiasi hiki, na si kutaka kufanya ujanja ujanja,” Msimamizi na Mwanasheria wa Ladack Chasambi wa Simba Sc.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live