Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msikie Manara akitaja thamani ya goli la Fei toto (+ Video)

Kiungo wa Yanga, Feisal Salum akifunga goli la pili la Yanga

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Oktoba 19, Yanga walikua ugenini kule Songea wakikipiga na KMC mchezo wa Ligi kuu na wakafanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-0.

Wafungaji wa magoli hayo ni Straika msumbufu na mwenye nguvu na kasi Fiston Mayele na Kiungo Feisal Salum "Fei Toto".

Leo hii Yanga wamerejea kutokea Songea kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Azam utakaopigwa katika Uwanja wa Mkapa Oktoba 30.

Sasa walipokuwa uwanja wa ndege, JNIA, Msemaji wa Yanga, Haji Manara alipata nafasi ya kuzungumza na vyombo vya habari, na katika mengi aliyoyazungumza ni pamoja na goli la Fei toto, akitaja ubora na thamani ya goli hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live