Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msigwa: Weledi utatuweka pazuri

Msigwa Mkutanoni Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa

Sun, 9 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa akimwakilisha waziri, Damas Ndumbaro katika mkutano mkuu wa mwaka wa Yanga 2024, amesisitiza juu ya weledi katika namna ya uendeshaji kwa klabu za Ligi Kuu Bara.

Msigwa amesema hayo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam wakati akiwapongeza viongozi Yanga kwa mageuzi makubwa ambayo wameyafanya.

"Kwa niaba ya Waziri naomba kuwafikishia salamu kwa kuwapongeza kwa ubingwa wa 30, amewapongeza pia kwa ubingwa wa FA, ameniambia niwaambie yupo pamoja nanyi," amesema Msigwa na kuongeza;

"Kwa dhati ya moyo wangu naomba kuwapongeza kwa mafanikio makubwa, upande wa wizara kwa niaba ya Serikali jambo muhimu ni namna Yanga mmetengeza weledi katika uendeshaji. Serikali tunatamani kuona klabu zikiwa na uendeshaji mzuri wa uendeshaji. Tunataka kywa sehemu ya mafanikio na sio usuluhishi wa migogoro. Naiona Sayansi kwenye klabu ya Yanga."

Msigwa alimalizia kwa kuwataka Yanga kuendelea kuwa mfano mzuri juu ya namna ya uendeshaji wa klabu; "Kuna mahali mmesogea, natamani kuona klabu za Tanzania ifike hatua ziwe kiuendeshaji sawa na klabu kubwa za soka Ulaya."

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alisema katika mkutano huo mara baada ya katibu huyo kuongea kuwa viongozi wa TP Mazembe walikuja nchini kwa ajili ya kuangalia namna ya uendeshaji wa klabu hiyo kutokana na kufanya kwao vizuri.

Kauli hiyo ilikuwa ni kama majibu kwa Msigwa kuonyesha kile ambacho wanafanya kimeanza kuonekana na kuigwa na klabu nyingine za ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: