Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshuti wa Fei Toto waitia hasara TFF

Mshuti Pic Data Kiungo wa Stars, Feisal Salum

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Achana na matokeo ya bao 1-1 iliyopata timu ya Taifa ya Tanzani ‘Taifa Stars’ dhidi ya Sudan Kusini kwenye mchezo wa kirafiki kujiandaa na mechi ya kufuzu AFCON, kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ amezua jambo.

Kiungo huyo fundi wa kupiga mashuti ya mbali amepoteza mpira wa Stars baada ya kupiga shuti kali lililotoka nje ya Uwanja wa JMK Park na kutokomea kusiko julikana.

Kwenye mchezo huo maalum kwaajili ya kujiweka fiti kuelekea mchezo wa kufuzu AFCON dhidi ya Somalia Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, Fei Toto akiwa kwenye harakati za kuifungia bao timu hiyo kwa shuti kali alijikuta mpira unapaa juu ya lango na kutoka nje.

Kwenye mchezo huo mshambuliaji Reliants Lusajo ndiye aliyeifungia Stars bao la kusawazisha baada ya kutanguliwa na Sudan Kusini mabao yote yalifungwa kipindi cha pili.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Kocha Mkuu wa Stars, Kim Poulsen alisema amebaini makosa yaliyofanywa na wachezaji wake kipindi cha kwanza wameanza mpira kwa kupooza na kufanya makosa mengi akitaja sababu kuwa ni kutoka mapumzikoni miili yao bado haijafunguka.

Alisema baada ya kubaini makosa hayo aliyafanyia kazi

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz