Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshindi wa kwanza wa Ballon d'Or Uhispania afariki dunia

Luis Suarez 88.jpeg Mshindi wa kwanza wa Ballon d'Or Uhispania afariki dunia

Mon, 10 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo wa zamani wa Barcelona na Inter Milan Luis Suarez,ni mchezaji wa kwanza mzaliwa wa Hispania kushinda tuzo ya Ballon D'Or, amefariki dunia jana Jumapili akiwa na umriwa wa miak 88

Kwa jina la utani "The Architect" Mhispania huyo alishinda tuzo hiyo ya kifahari mwaka wa 1960 na baadaye akawa kocha wa La Roja kwenye Kombe la Dunia la 1990.

"Luis Suarez Miramontes amefariki Jumapili leo mjini Milan akiwa na umri wa miaka 88," imesema taarifa ya Barcelona.

"Aliichezea Barca kati ya 1954 na 1961 kabla ya kwenda Inter Milan, ambako pia ni gwiji wa mpira."

Suarez alipendwa sana nchini Italia baada ya kuwa mmoja wa viungo wa kati walioshangiliwa zaidi kwenye ligi akiwa Inter Milan chini ya kocha Helenio Herrera miaka ya 1960, ambaye alimfuata kutoka Barcelona.

"Kifo chake kinatuachia huzuni kubwa -- hamu ya soka yake kamilifu na isiyoweza kuepukika, ambayo ilihamasisha vizazi, inawekwa kwenye kumbukumbu kuwa mwanasoka wa kipekee na mchezaji mkubwa wa Inter," imeandika Inter katika taarifa.

Suarez, aliyezaliwa La Coruna mnamo 1935, alianza uchezaji wake huko Deportivo La Coruna, kabla ya kuhamia Barcelona mnamo 1954.

Alishinda mataji mawili ya La Liga akiwa na wababe hao wa Catalan, kati ya fedha nyingine na kushinda Ballon d'Or.

Mchezaji mwingine pekee aliyezaliwa Uhispania kushinda tuzo ya Ballon d'Or ni kiungo wa Barcelona Alexia Putellas, ambaye ameshinda kombe la wanawake mara mbili.

Alfredo Di Stefano, ambaye aliichezea Argentina na baadaye timu ya taifa ya Uhispania, alishinda mara mbili lakini alizaliwa Buenos Aires.

"Suarez alikuwa mchezaji mzuri sana, kati ya Wahispania bora kuwahi kutokea katika historia, pamoja na Xavi (Hernandez) na (Andres) Iniesta," amesema Di Stefano katika mojawapo ya mahojiano yake ya mwisho kabla ya kifo chake mwaka 2014.

Chanzo: Mwanaspoti