Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshindi wa Kombe la Dunia England 1966 afariki

Skynews Obit George Cohen 6004882 George Cohen

Fri, 23 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa beki wa kulia katika timu ya England, iliyoshinda Kombe la Dunia mwaka 1966, George Cohen amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 83, klabu yake ya zamani ya Fulham imetangaza.

Fulham wametangaza taarifa hiyo kupitia kwenye akaunti yao rasmi ya Twitter "Kila mtu katika klabu ya Soka ya Fulham amehuzunishwa sana kusikia kifo cha mmoja wa wachezaji wetu bora kabisa,George Cohen"

Uchezaji wake wa kuvutia ulimfanya acheze kwa mara ya kwanza katika timu ya Taifa ya England mnamo Mei 1964 wakati wa ushindi wa 2-1 dhidi ya Uruguay kwenye uwanja wa Wembley.

Cohen alijidhihirisha kuwa chaguo la kwanza la beki wa kulia wa nchi yake na alicheza kila dakika ya kampeni za ushindi za England za Kombe la Dunia 1966, zikiwemo dakika zote 120 za ushindi wa 4-2 dhidi ya Ujerumani kwenye fainali.

Cohen alilazimika kustaafu akiwa na umri wa miaka 29 kutokana na jeraha la goti na baadae alifanya kazi kama kocha katika timu ya vijana ya Fulham na U23.

Mchango wake kwa Fulham ulitambuliwa mwaka wa 2016 walipotangaza kujenga sanamu yake kwenye wa Craven Cottage na ilizinduliwa Oktoba mwaka huo.

"Tuna huzuni sana kusikia habari za kifo cha George Cohen leo," alisema Mwenyekiti wa FA, Debbie Hewitt

Sir Geoff Hurst, ambaye alifunga hat-trick katika ushindi wa fainali ya Kombe la Dunia la England, alisema: "Inasikitisha sana kusikia rafiki yangu na mchezaji mwenza wa timu ya Uingereza George Cohen amefariki"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live