Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshindi AFCON 2024 kuondoka na kitita hiki...!

Winner AFCON 2024 Mshindi AFCON 2024 kuondoka na kitita hiki...!

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika CAF, leo limetangaza ongezeko la 40% la Pesa kwa Mshindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika la TotalEnergies (AFCON) litakalofanyika nchini Côte d’Ivoire kuanzia wiki ijayo.

Mshindi wa TotalEnergies AFCON Côte d’Ivoire 2024 atapokea dola za Kimarekani USD 7 000 000, sawa na Shilingi za Tanzania Bilioni 17.6

Mshindi wa Pili wa mashindano hayo makubwa barani Afrika sasa atapata USD 4 000 000, sawa na TSh. Bilioni 10. Kila mmoja wa Washindi wawili wa Nusu Fainali atapata (USD 2 500 000) sawa na Shilingi Bilioni 6 na kila mmoja kati ya wanne waliofuzu Robo Fainali (USD 1,300,000) zaidi ya TSh. Bilioni 3.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live