Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshery hana hofu Yanga

Mshery Mshery hana hofu Yanga

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa wa Yanga, Aboutwalib Mshery amesema hana presha juu ya uwepo wa kipa mpya kikosini hapo, Metacha Mnata aliyesajiliwa ghafla siku ya mwisho ya usajili wa dirisha dogo, Januari 15, mwaka huu baada ya Mshery kuumia.

Yanga ilimrejesha Mnata kikosini dakika chache kabla ya usajili wa Januari kufungwa akitokea Singida Big Stars kwa mkopo wa miezi sita baada ya taarifa ya daktari kueleza Mshery atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi kisichopungua miezi miwili jambo liliwafanya Wanajangwani hao kutafuta mbadala.

Mshery anafahamu kwamba benchi la ufundi la Yanga linaweza kuvutika kumuongeza mkataba Metacha kama ataonyesha mambo makubwa, lakini ameiambia Mwanaspoti, kuwa uwapo wa kipa huyo ni faida kwa Yanga na yeye binafsi.

“Taratibu napona, muda ukifika nitarejea uwanjani. Nafurahi kuona timu yangu inafanya vizuri na eneo langu la golini, kumekuwa imara,” alisema Mshery na kuongeza;

“Uwepo wa Mnata ni jambo zuri kwa timu, hata kwangu. Kwanza inaongeza uhakika wa eneo lile kwani tupo makipa wanne sasa na kila mmoja ana ubora wake pia tutakuwa tukielekezana na kufundishana baadhi ya mambo.”

Kipa huyo aliyetua Yanga kutoka Mtibwa Sugar, bado anatembea kwa msaada wa magongo baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti, mwezi uliopita nchini Tunisia. Yanga sasa ina makipa wanne akiwamo Djigui Diarra, Mnata na Eric Johora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live