Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshery awaita mashabiki Mkwakwani

Mshery Msks Aboutwalib Mshery

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa wa Yanga, Aboutwalib Mshery, amewaita mashabiki wajitokeze katika Dimba la Mkwakwani kwa ajili ya mchezo wa Ligi dhidi ya Coastal Union utakaopigwa kesho dimbani hapo.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji, Mshery alisema: “Kwa niaba ya wachezaji wenzangu, kutokana na mchezo wa kesho, tungeomba mashabiki wetu wa Yanga waliopo Tanga na mikoa ya karibu na hapa waweze kujitokeza kwa wingi kwa sababu kwa sasa hivi kila mechi ni muhimu sana kupata pointi tatu kuelekea kuchukua ubingwa.

“Sio Coastal Union tu, naamini kila timu ya chini inapokutana na timu kubwa inacheza vizuri sana kwa sababu wanataka matokeo mbele yako, kwa hiyo sio Coastal tu, bali timu yoyote tutakayokutana nayo tutapambana vilevile kusaka ushindi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live