Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshery: Yanga haina presha ya ubingwa

Msherya Mshery: Yanga haina presha ya ubingwa

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Ihefu huku watani wao, Simba wakishinda na kukaa kileleni mwa Ligi Kuu, Kipa wa Yanga, Abdultwalib Mshery amesema timu yao haina presha kwa kupoteza mchezo mmoja huku akitamba kwamba mbio za ubingwa bado ni mapema kukata tamaa.

Yanga iliyokuwa kileleni kwa pointi tisa ilikubali kichapo cha mabao 2-1 mbele ya Ihefu huku Simba ikishinda kwa mabao 3-1 mbele ya Tanzania Prisons na kukaa kileleni ikifikisha pointi 12 huku Yanga ikisalia na alama tisa katika nafasi ya tatu na Azam yenye pointi 10 ikikamata nafasi ya pili.

Yanga itakuwa na nafasi ya kujisahihisha kesho na kufufua matumaini itakapovaana na Geita Gold kuanzia saa 10 jioni katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Akizungumza leo Oktoba 6, 2023 jijini Mwanza, Mshery amesema mashabiki wa Yanga hawawezi kukata tamaa kwa matokeo ya mchezo mmoja pekee, huku akitamba kwamba kikosi chao kitainuka na kurejea katika nafasi yake kama zinavyofanya siku zote timu kubwa kote duniani.

"Tunapaswa kuonyesha kesho maana halisi ya timu kubwa bila kujali inayoyapitia inahitaji kurudi na kupata matokeo. Kwa hiyo tutatuliza akili tutajipanga na kufanya vizuri kesho," amesema Mshery.

"Mashabiki wa Yanga hawawezi kukata tamaa kwa mechi moja kwa sababu wana imani kubwa na timu yao. Hakuna presha yoyote kwa sababu ligi bado mapema huhitaji kujipa presha kwa mechi moja. Hata hivyo hii ni kengele imetushtua kwamba tuamke na kufanya vizuri."

Akizungumzia mchezo wa kesho, Mshery amesema tayari benchi la ufundi limeshafanya kazi yake na wachezaji wamezungumza kuhakikisha hawafanyi tena makosa katika mchezo huo ili kuwapa furaha mashabiki wao.

"Wachezaji tumezungumza, mechi iliyopita tulipoteza tunajua umuhimu wa mchezo wa kesho hivyo tunahitaji kushinda na kupata alama tatu. Kama wachezaji tunazingatia kile ambacho mwalimu anatuambia kwa sababu yeye ndiye anaona kiufundi na kujua nini tunapaswa kufanya," amesema kipa huyo.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: