Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshery: Tunazitaka tatu za Coastal Union

Mshery  1024x1024 Mshery: Tunazitaka tatu za Coastal Union

Fri, 26 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipa wa Yanga SC, Aboutwalib Mshery, amezungumzia umuhimu wa mchezo wa Kesho Jumamosi dhidi ya Coastal Union tunaotarajia kucheza kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC, utaanza saa 12:00 jioni ambapo timu ya Young Africans SC itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kushinda goli 1-0 katika mzunguko wa kwanza tukiwa ugenini dhidi ya wapinzani wetu hao.

“Maandalizi yako poa, kilichotokea mchezo uliopita hakijatuathiri chochote, tupo vizuri kwa ajili ya kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Coastal Union.

“Pointi tatu ni muhimu sana kwa sababu tupo kwenye mbio za kuwania ubingwa, tutajitahidi mchezo unaofuata kupata matokeo ya ushindi yatakuwa muhimu sana kwetu.

“Huwezi kuchukua ubingwa kama utaogopa kukutana na timu ngumu, Coastal wapo kwenye ubora na sisi tupo katika kuufukuzia ubingwa, kwa hiyo ubora wa Coastal ndio changamoto kwetu ya kwenda kuchukua ubingwa.

“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa sababu mchezo huu ni muhimu sana, tokea mchezo uliopita hatukuwa na matokeo mazuri kwa hiyo sapoti yao ni muhimu sana,” alisema Mshery.

Viingilio vya mchezo huo ni Tsh 20,000 kwa Jukwaa la VIP A, VIP B Tsh 10,000 na Mzunguko Tsh 5,000.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live