Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshambuliaji wa Yanga ajiunga na Al Nassr ya Ronaldo

Luvanga (76).jpeg Clara Luvanga.

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani wa Yanga Princess na timu ya taifa, Clara Luvanga ameingia mkataba wa miaka mitatu na timu ya soka ya wanawake ya Al Nassr kutoka Saudi Arabia.

Ni miezi miwili tu imepita baada ya kusajiliwa na Dux Lugrono ya Hispania na miamba hiyo ya soka ya Saudia kuvunja mkataba wake na timu hiyo.

Clara alianza vyema kwenye Ligi ya Hispania na kuifungia timu yake bao moja iliposhinda mabao 7-0 na huenda Nassr walivutiwa na kiwango alichoonyesha straika huyo.

Mtu wa karibu wa mchezaji huyo amebanisha kuwa bado kukamilisha taratibu za kiafaya na ikikamilika muda wowote Clara atatambulishwa.

"Mwanzo ilikuwa England, Saudia na Sweden ndio zilikuwa zinamuhitaji lakini tuliangalia pesa ndefu bado kuna vitu vidogo kukamilika na muda wowote mambo yatakuwa safi," amesema mtu huyo.

Kwa mkataba huo utamfanya Clara anunuliwe kwa Sh250 milioni na kuingiza mshahara wa zaidi ya milioni 16 kwa mwezi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: