Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mshahara wa De Gea ndo tatizo

David De Gea Record David De Gea

Mon, 5 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Inaelezwa kipa wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Hispania, David De Gea anashindwa kujiunga na timu kibao kwa sababu ya mshahara wake mkubwa.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya TEAMtalk, kinachomkwamisha De Gea asipate timu hadi sasa ni kutaka kwake kuendelea kusalia katika soka la kiushindani na timu nyingi kushindwa kufikia mwafaka juu ya masuala yake ya mishahara.

De Gea ambaye amekuwa nje ya uwanja msimu mzima tangu aondoke Old Trafford, amekuwa akisakwa na timu kibao za Saudi Arabia na Marekani.

Hadi sasa ametimiza siku 430 nje ya uwanja baada ya kudumu kwa miaka 12 akiwa kipa namba moja wa timu hiyo, kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Andre Onana.

Kabla ya kuachwa De Gea alikubali kukatwa mshahara wake wa Pauni 3750,00 hadi Pauni 200,000 kwa wiki lakini Man United ilimwambia asubiri kwanza wakati wanafikiri ikiwa wanaweza kuendelea naye ama watamuacha, hata hivyo, aliachwa.

Timu mbalimbali ikiwemo Newcastle, Nottingham Forest, Real Betis na baadhi kutoka Saudi zilijaribu kumpa ofa ya kutaka kumsajili dirisha la majira ya baridi lakini alikataa.

Katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu timu kutoka Italia ikiwamo Genoa na Fiorentina lakini ameshindwana nazo kutokana na masuala ya mishahara.

Pia inaelezwa baadhi ya timu za Saudia na Marekani ziko tayari kumpa mshahara anaohitaji lakini hayupo tayari kuondoka katika soka la kushindani kwa sasa.

Hivi karibuni aliziambia Genoa na Fiorentina anataka mshahara wa Pauni 5 milioni kwa mwaka ambao ni sawa na Pauni 80,000 kwa wiki.

Kiasi hicho cha pesa kilionekana ni kikubwa na timu hizo zilikuwa zikihitaji kulipa Pauni 4 milioni mwaka kiasi ambacho yeye alikikataa.

Chanzo: Mwanaspoti