Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mserbia wa Tabora United aonya mastaa

Goran Kopunovic 09 14.jpeg Mserbia wa Tabora United aonya mastaa

Sat, 28 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Tabora United Mserbia, Goran Kopunovic amewakata wachezaji wa timu hiyo kuongeza umakini zaidi na kuepuka makosa yanayoweza kuwagharimu wakati kikosi hicho kitakapopambana na Kagera Sugar kesho katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba unazikutanisha timu zote ambazo zimepoteza mechi zao za mwisho ambapo Kagera ilichapwa bao 1-0 na Dodoma jiji, sawa na Tabora pia iliyofungwa 1-0 na Maafande wa JKT Tanzania.

"Tumekuwa na siku chache za kurekebisha kasoro ndogondogo zilizojitokeza katika mchezo wetu wa mwisho na nawashukuru wachezaji wameonyesha kuguswa hivyo kuniahidi kupambana zaidi kadri ya uwezo wao ili tupate matokeo mazuri," alisema.

Goran aliongeza kupata pointi moja kati ya sita katika michezo miwili iliyopita sio jambo nzuri hivyo anahitaji kuona hali hiyo ikibadilika kwani bila ya kuweka mikakati mizuri hawawezi kufikia malengo waliyojiwekea ya kumaliza nafasi nne za juu.

"Kila mmoja wetu ana malengo aliyojiwekea na licha ya kucheza kwa msimu wetu wa kwanza hatuwezi kujishusha kwa sababu tuna wachezaji wazuri wenye uwezo mkubwa ambao sisi kama benchi la ufundi tunaamini wanaweza kufanya mambo makubwa."

Katika michezo saba ambayo timu hiyo imecheza imeshinda miwili, sare mitatu na kupoteza miwili ikiwa nafasi ya saba na pointi tisa.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: