Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mserbia aifuata Ihefu kimkakati

Goran Kopunovic 09 14.jpeg Kocha Mkuu wa Tabora United, Mserbia Goran Kopunovic

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Tabora United, Mserbia Goran Kopunovic amewakata wachezaji wa timu hiyo kuongeza umakini zaidi na kuepuka makosa yanayoweza kuwagharimu wakati kikosi hicho kitakapopambana na Ihefu kesho katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Highlands Estate, Mbeya unazikutanisha timu zote ambazo hazijashinda mechi zao zilizopita ambapo Ihefu ililazimishwa suluhu na Tanzania Prisons huku Tabora ikifungana bao 1-1 na Mashujaa.

“Tumekuwa na siku chache za kurekebisha kasoro ndogondogo zilizojitokeza katika mchezo wetu wa mwisho na nawashukuru wachezaji wameonyesha kuguswa hivyo kuniahidi kupambana zaidi kadri ya uwezo wao ili tupate matokeo mazuri,” alisema.

Goran aliongeza kupata pointi moja ugenini dhidi ya Mashujaa sio jambo baya kwao ingawa anahitaji kuona mabadiliko ya kiuchezaji kwa wachezaji wa kikosi hicho hasa katika utumiaji wa nafasi vizuri kwenye kufunga na katika kuzuia pia.

“Tunatambua wapinzani wetu hawako kwenye wakati mzuri lakini tunaenda kucheza kwa tahadhari zote kwa sababu michezo hii huwa haitabiriki kirahisi, tunawaheshimu sana ila malengo yetu kwa michezo miwili ugenini ni kupata angalau pointi nne.”

Katika michezo 11 iliyocheza timu hiyo imeshinda 3, sare sita na vipigo 2.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: