Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msemaji Vital'O: Tunawaogopa Diarra, Aziz, Pacome na Maxi

Yanga Arsene Pacome Aziz Ki Msemaji Vital'O: Tunawaogopa Diarra, Aziz, Pacome na Maxi

Wed, 14 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa timu ya Vital’O ya Burundi umewataja wachezaji wa Yanga SC, kipa Djigui Diarra na viungo Max Nzengeli na Stephane Aziz KI kama kizingiti kwao kuwatoa Yanga SC katika Mashindano ya CAF.

Uongozi huo umesema wachezaji hao ni msaada mkubwa kwa kikosi hicho na kueleza kuwa mchezo wao wa Klabu Bingwa Jumamosi utakuwa mgumu kutokana na nyota hao.

Akizungumza na Manara TV baada ya kuwasili nchini, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa timu hiyo Arsene Bucuti alisema nyota hao ni moto, lakini watapambana.

“Kwanza tunamhofia Diarra, ni kipa mgumu kufungwa kwa hapa Tanzania hata kama wanamfunga AFCON. Wengine ni Maxi Nzengeli, Aziz Ki, Pacome Zouzoua. Ni wachezaji professional, ni wachezaji ambao wanajua wanachokifanya.

“Zamani mashabiki wa Tanzania walikuwa wanapenda Vital’O kuliko Simba na yanga, kwa hiyo tunao mashabiki wa kutosha hapa Tanzania. Tumeshawahi kuwapiga bao 7-0, sasa tunataka kurudia tulichokifanya zamani,” amesema Arsene.

Timu hizo zitacheza pambano lake Jumamosi katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: