Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msemaji Vital'O: Simba alipigwa 5, Azama akala 4, tuungane kuinyamazisha Yanga

Baccuti A48DC.jpeg Arsene Bucuti

Wed, 21 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa timu ya Vital'O Fc, Arsene Bucuti amewaomba vilabu vya Tanzania ikiwe Simba SC, Azam FC na vingine kuunganisha nguvu na kuwapa sapoti timu yake ili waweze kuifunga Yanga SC kwenye mchezo wao wa marudiano na wafanikiwe kuitoa katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Yanga Sc kwenye mchezo wao wa awali wa Michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika waliifunga Vital'O mabao 4-0 katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi na sasa watarudiana tena tarehe 24 Agosti,2024.

“Kwa sasa ninatembea maeneo mbalimbali ya Dar kutafuta mashabiki wa Simba, Azam, Namungo, KMC, Pamba Jiji waje kwenye uwanja, tunaenda kumalika kazi tunapindua meza. Kile mlichokiona mchezo wa kwanza yalikuwa makucha ya mkono mmoja, mechi ya marudiano tutakunjua makucha yote, nawaambia mtaona maajabu.

“Magari zaidi ya 50 yametoka nchini Burundi kuja Dar kushuhudia mchezo huo. Sisi Warundi hatupendi aibu, hatupendi tupigiwe Tanzania. Rais wetu hapendi dharau, Waziri mkuu na meya wetu hawapendi dharau, hawawezi kukubali. Yanga kutupiga bao 4-0 ile ni dharau.

“Yanga alitufunga sisi bao 4 lakini Simba alichapwa bao sita saba, maana yake Vital’O ni wazuri kuiliko Simba. Ndiyo maana tunatafuta sapoti kwa Simba na Azam tuungane tupindue meza Yanga afungwe.

“Yanga ilivyotufunga bao 4 nikakumbuka Yesu alivyotundikwa msalabani, lakini nikaona Yesu alifufuka siku ya tatu, na sisi tutafufukia kwenye Uwanja wa Mkapa pale. Sisi mambo tumeshamaliza, mabao matano tu.

“Kama Mlandege inaipiga Yanga kwa nini Vital’O isimpige Yanga, leo nakwenda Unguja kwa wazee wangu kuwauliza ni jinsi gani huwa wanaweza kuwafunga Yanga na Simba na Azam,” amesema Baccuti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: