Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msemaji Singida: Mechi ya Yanga haikuwa ngumu

Guede Aziz Ki Sdv Msemaji Singida: Mechi ya Yanga haikuwa ngumu

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga SC wanaondoka na faida ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida Fountain Gate kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Ni kwenye SportPesa Dabi Yanga wameibuka wababe kwa kukomba pointi tatu muhimu kwenye mchezo huo baada ya dakika 90.

Joseph Guede ameandika rekodi ya kufunga mabao mawili dakika ya 41 na dakika ya 68 huku bao moja likifungwa na Aziz KI dakika ya 66.

Akizungumzia mchezo huo, Msemaji wa Singida Fountain Gate FC, Hussein Masanza amesema kuwa mechi hiyo haikuwa ngumu lakini makosa ya wachezaji ndiyo yalisababisha wakose ushindi.

“Mechi ya leo haikuwa ngumu kabisa, kwa mtu aliyefika katika Dimba la CCM Kirumba au ametazama kwenye TV atakubaliana na mimi kwa sababu timu imecheza vizuri na wachezaji walionekana wanafuata maelekezo ya mwalimu ipasavyo na wanautaka ushindi kama timu.

“Kwa nini tumefungwa licha ya kucheza vizuri? Nimezungumza na mwalimu amesema hakuona tatizo lolote kwenye game plan ama wachezaji kujitoa na amewapongeza sana lakini mwalimu amesikitishwa na makossa yaliyofanywa na wachezaji.

“Yapo makossa ambayo yamefanywa na mchezaji mmoja mmoja tena ni ya kizembe kabisa wala sio ya kiuwezo mpaka wakaruhusu tukashambuliwa na kufungwa mabao matatu.

“Kwa hiyo mchezo haukuwa mgumu lakini tumepoteza kutokana na makossa ambayo yamefanywa na wachezaji na hayo lazima yaende kushughulikiwa kiufundi,” amesema Msanza.

Singida Fountain Gate ipo nafasi ya 9 kwenye msimamo ikiwa na pointi 24 baada ya kucheza mechi 22 msimu wa 2023/24.

Ikumbukwe kwamba Singida Fountain Gate wamepoteza pointi zote sita mbele ya Yanga, mzunguko wa kwanza ubao ulisoma Yanga 2-0 Singida Fountain Gate.

Yanga inafikisha jumla ya pointi 55 baada ya kucheza mechi 21 ndani ya ligi kituo kinachofuata ni Kariakoo Dabi dhidi ya Simba, Aprili 20 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live