Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Msauzi wa Singida FG akerwa, awawakia mastaa

Thabo Senong Kocha Mkuu wa Singida Fountain Gate, Thabo Senong

Sat, 17 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Matokeo ya kupoteza mechi mbili mfululizo yameonekana kumkera Kocha Mkuu wa Singida Fountain Gate, Thabo Senong, raia wa Afrika Kusini, aliyedai nyota wake kufanya makosa binafsi huku akitaja kuondoka kwa wachezaji saba wakati dirisha dogo nako kumechangia.

Singida FG imepoteza mechi mbili mfululizo ikiruhusu mabao manne, ikianza kulazwa 1-0 na Kagera Sugar kabla kuchakazwa 3-1 na Tanzania Prisons.

Timu hiyo iliyowahi kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita, katika dirisha dogo iliwaachia nyota tisa wakiwamo wawili waliotolewa kwa mkopo Meddie Kagere (Namungo) na Gadiel Michael (Cape Town Spurs ya Sauzi.

Wachezaji waliopigwa bei ni Elvis Rupia, Duke Abuya, Morice Chukwu, Joash Onyango, Mukrim Issa, Morouf Tchakei na Khomein Aboubakari waliotimkia Ihefu.

Senong alisema katika mechi hizo hajafurahishwa na matokeo hayo kwani wachezaji walionyesha viwango duni wakifanya makosa binafsi na kutotumia nafasi walizopata.

Alisema hata kuondoka kwa nyota tisa kumechangia kwani benchi la ufundi imewapa wakati mgumu kuanza kusuka upya timu na kutoa matumaini kuwa wataimarika kwani bado mechi zipo.

“(wachezaji) wamefanya makosa binafsi. Wanakosa umakini kutumia nafasi walizopata kufunga mabao. Nyota walioondoka wameweka pengo na kufanya benchi la ufundi kuanza kusuka upya,” alisema.

“Bado tuna mechi nyingi ikiwamo za Kombe la Shirikisho tutakaa na wachezaji kusahihisha makosa ili kuweza kushinda michezo inayofuata kwenye mashindano yetu.”

Kwa upande wake kipa Beno Kakolanya alisema kufungwa mabao matatu katika mchezo mmoja siyo matokeo mazuri akieleza kuwa makosa waliyofanya benchi la ufundi litafanyia kazi.

“Tuwatoe hofu mashabiki bado tuna mechi nyingi ikiwamo Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), hivyo tutasahihisha makosa haya na tutafanya vizuri hatuwezi kupoteza malengo yetu,” alisema Kakolanya.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: