Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrithi wa Tuisila Hakamatiki

Moloko Pic Ducapel Moloko

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni suala la muda tu kabla ya Timu ya Yanga kushusha kifaa kingine kipya ambacho kinasemwa kitakuja kuziba nafasi ya winger mwenye kasi ya ajabu Tuisila Kisinda "TK Master".

Yanga imeshaweka mambo sawa na winga Mkongomani, Ducapel Moloko ambaye ni mbadala wa Tuisila Kisinda ambaye muda wowote kuanzia sasa atasaini mkataba na Berkane ya Morocco.

Moloko inadaiwa kuwa ameshafanya mazungumzo na Yanga na amewaambia wampe wiki moja tu aweke ishu zake sawa ajiunge nao kambini, kama muda utakua unaruhusu anaweza kuwahi hata safari ya Morocco..

Moloko ambaye ana uwezo mkubwa wa kusukuma mashambulizi na kufunga msimu huu.

Mmoja wa viongozi wa Yanga alidokeza jana kwamba dili hilo litakuwa sapraizi kwa mashabiki na wanaamini kwamba mchezaji huyo ni sahihi kwa mahitaji ya Kocha Mkuu wa Yanga Mohammed Nabi.

Moloko ndiye mchezaji aliepewa nafasi baada ya Kisinda kuondoka AS Vita na habari zinasema kwamba Mukoko Tonombe amehusika kumpendekeza. Habari zinasema kwamba Moloko anaweza kujiunga na timu hiyo dakika za mwisho jijini Dar es Salaam kabla ya kukwea pipa kwenda kambini Morocco au akichelewa ataunganisha juu kwa juu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live