Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrithi wa Metacha asaini miwili Yanga

Metacha X Khomeny Mrithi wa Metacha asaini miwili Yanga

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga imepata mrithi wa kipa Metacha Mnata, ambaye ni Abubakar Komeni wa Ihefu na bila kuchelewa tayari imeshamsainisha mkataba wa miaka miwili.

Komeni ambaye alikuwa amebakiza mkataba wa mwaka mmoja na Singida Black Stars, alipelekwa Ihefu kwa mkopo wa miezi sita dirisha dogo.

Taarifa za ndani zimeliambia Mwanaspoti kuwa; “Kipa huyo ni kweli amesaini mkataba wa miaka miwili na Yanga itamtangaza hivi karibuni na wanachosubiri ni muda tu ila ilishamalizana kila kitu na uongozi wa mchezaji huyo.”

KWANINI KOMENI

Jambo lililopelekea uongozi wa timu hiyo kufikiria kumsajili kipa mwingine ni mzawa ni baada Metacha kuwa na rekodi zisizoridhisha mara kwa mara.

Yanga haikutaka kusajili kipa wa kigeni kwani idadi ya wachezaji hao ilikuwa imekwisha kutimia,licha ya ubora mkubwa aliouonyesha Dijgui Diarra ndani ya misimu mitatu aliyochezea kikosi hicho.

Hapo ndipo walipomgeukia kipa wa Tanzania Prisons Yona Amosi, lakini uongozi wa kikosi hicho ulipogundua mpango huo ulimuongeza mkataba wa miaka miwili haraka.

Baada ya hayo jina la kipa Beno Kakolanya liliwekwa mezani na kuwagawanya viongozi, wengine walimkataa kutokana na rekodi mbaya ya utovu wa nidhamu aliyokuwa alipokuwa na Yanga na hata alipotoka katika timu hiyo.

Ndipo ilipoamua kutimkia Ihefu kwa kipa wao Abubakar Komeni na mwisho waliweza kukamilisha dili hilo kwa kupata saini yake tayari kwa kuitumikia Yanga miaka miwili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live