Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrithi wa Klopp asema fresh

Amorimm (5).jpeg Mrithi wa Klopp asema fresh

Tue, 9 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Sporting Lisbon, Ruben Amorim ambaye anahusishwa sana na Liverpool katika siku za hivi karibuni amesema ni kweli anaweza kuondoka timu hiyo mwisho wa msimu huu.

Kwa sasa Liverpool ipo katika mawindo ya kocha mpya ili kuziba pengo la Jurgen Klopp ambaye ataondoka mwisho wa msimu huu.

Awali, Liverpool ilikuwa ikihusishwa sana na kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso lakini wiki iliyopita alisema ataendelea kuwepo Leverkusen kwa msimu ujao.

Baada ya kauli hiyo nguvu zote sasa zinaonekana kuhamishiwa kwa Amorim, 39, na kocha huyo ameweka wazi kwamba hana shida yoyote juu ya kuondoka.

“Siwezi kuahidi kama nitaendelea kuwepo Sporting kwa msimu ujao, tuna muda wa kujadili juu ya hatma yangu, nitajadiliana na mabosi muda sahihi ukifika, kwa sasa nguvu zangu nimeziwekeza kwenye kushinda mataji na baada ya hapo tunaweza kuona nini kinafuata” alisema Amorim alipoulizwa juu ya hatma yake na tetesi za kuhitajika na Liverpool.

“Sporting ndio ina hatma yangu, siwezi kufanya uamuzi wowote kwa sababu niliwapa ahadi kwamba kama sijashida mataji basi nitaondoka.”

Amorim ana mkataba wa kuendelea kusalia kwenye viunga vya Sporting hadi mwaka 2026, hivyo ili kumpata itatakiwa Liverpool itatakiwa kuvunja mkataba wake.

Sporting kwa sasa ndio vinara wa Ligi Kuu Ureno ikiwa inaongoza kwa tofauti ya alama moja dhidi ya Benfica.

Inaonekana kuna urahisi wa kumpata Amorim kwa sababu ya uhusiano wa mabosi wa Liverpool na wakala wake Raul Costa ambaye pia ni wakala wa winga wao Luis Diaz na alihusika kwenye mazungumzo ya kukamilisha dili hilo.

Chanzo: Mwanaspoti