Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrithi wa Klopp... Kama sio Alonso basi ni De Zerbi

Xabi Alonso .jpeg Mrithi wa Klopp... Kama sio Alonso basi ni De Zerbi

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Liverpool imeripotiwa kumwongeza Roberto De Zerbi kwenye orodha ya makocha watatu inaowataka waje kuziba pengo la Jurgen Klopp endapo itamkosa Xabi Alonso.

Msako wa kocha mpya unaendelea huko Anfield ili kujiandaa na msimu ujao, ambapo Klopp atafungasha virago vyake na kuondoka msimu huu utakapofika tamati.

Kiungo wa zamani wa Liverpool, Alonso amewekwa kwenye chaguo la kwanza baada ya kufanya vyema huko Bayer Leverkusen. Mhispaniola huyo mwenye umri wa miaka 42, kwa sasa timu yake inaongoza kwenye msimamo wa Bundesliga, pointi saba juu ya Bayern Munich kabla ya mechi ya jana Jumapili, hivyo imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kubeba taji la ligi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 120.

Lakini, Barcelona na Bayern nazo zinahitaji makocha wapya, hivyo Liverpool inatambua upinzani unaowakabili kwenye kumpata Alonso.

Hilo ndilo linalowafanya Kop kufikiria machaguo mengine na ndiyo maana, De Zerbi amewekwa kwenye orodha. Mtaliano huyo amekuwa akifanya vizuri tangu alipotua Brighton kuchukua mikoba ya Graham Potter.

Ukimweka kando De Zerbi, makocha wengine waliopo kwenye rada za Liverpool ni Amorim, 39, wa Sporting Lisbon, ambaye aliipa ubingwa wa ligi kwenye msimu wake wa kwanza na msimu huu anachuana jino kwa jino na Benfica. Kocha mwingine ni Julian Nagelsmann, kocha wa zamani wa Bayern Munich.

REKODI ZA DE ZERBI

-Darfo Boario - mechi 22, ushindi 5, sare 5, vichapo 12

-Foggia - mechi 91, ushindi 47, sare 25, vichapo 19

-Palermo - mechi 13, ushindi 1, sare 3, vichapo 9

-Benevento - mechi 29, ushindi 6, sare 3, vichapo 20

-Sassuolo - mechi 120, ushindi 43, sare 36, vichapo 41

-Shakhtar Donetsk - mechi 30, ushindi 20, sare 5, vichapo 5

-Brighton - mechi 75, ushindi 35, sare 19, vichapo 21

Chanzo: Mwanaspoti