Taarifa zilizotufikia zinaeleza kuwa Klabu ya Simba SC huenda ikampa kipaumbele Kocha Omar Najhi (wa pili kutoka kushoto) kuwa Kocha wao Mkuu akirithi pahala pa Abdelhack Benchikha aliyojiengua kikosini wiki iliyopita.
Omar ni kocha kijana aliyefanya kazi na timu nyingi lakini zaidi alikuwa ni msaidizi wa kwanza wa Kocha Walid Regragui wa timu ya Taifa ya Morocco (Wakiwa Wydad) ambapo walifanya kazi kwa pamoja kwenye Michezo 48 ya klabu hiyo sanjari na Kocha wa Sasa wa Makipa wa Yanga (Mwenye miwani) Alaa El Meskini ambapo walishinda ubingwa wa Ligi Kuu Morocco na Ligi ya mabingwa barani Afrika.
Fahamu machache kuhusu Omar Najhi; - Ni mzaliwa wa England na raia wa England na Morocco - Amezaliwa 22 Machi 1978 - Aliachana na Tanger Januari 2024 kutokana na mdororo wa matokeo - Alikuwa Wydad kama msaidizi wa Regragui alikojiunga nao akitokea Mouloudia Oujda - Ni kocha mwenye vyeti halisi stahiki vya kusimama kama Kocha Mkuu.
Kocha huyo alipoulizwa kuhusu hilo amesema tujipe muda. Kwa sasa si muda muafaka kuzungumzia suala hilo ingali hawezi kukataa au kukubali chochote.