Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mrisho Ngassa aanika sababu za kuondoka Azam FC

Dew Ngassa Mrisho Ngassa aanika sababu za kuondoka Azam FC

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo Mshambuliaji wa wa zamani wa Yanga SC, Azam FC na Simba SC kwa nyakati tofauti, Mrisho Khalfan Ngassa amesema kuwa kilichosababisha akaondoka Azam ilikuwa ni baadhi ya viongozi wa klabu hiyo kumtuhumu kuwa ana mahaba na Yanga na anashindwa kuitumikia klabu yake hiyo ipasavyo.

Ngassa ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa Timu ya taifa ya Tanzania, taifa Stars amesema hayo wakati akifanyiwa mahojiano maalum na kipindi cha Salama Na... kinachoendeshwa na mtangazaji Salama Jabir.

"Niliondoka Azam FC kwa sababu viongozi wa Azam walikuwa wakinishutumu kuwa mimi ni Yanga. Ndio, mimi ni Yanga lakini majukumu Yangu nilikuwa nayafanya vyema.

"Sikutaka kuongeza mkataba Azam kwa kuwa niliona wananikosea heshima, ilifika kipindi viongozi walikuwa wanamfata kocha wanamwambia asinipange tunapocheza na Yanga. Kocha alitaka nicheze lakini viongozi walikataa asinipange kikosini.

"Ilikuwa Julai 28, 2012, Mchezo wa nusu fainali Kagame Cup dhidi ya AS Vita, nakumbuka nilifunga bao, tulishinda (2-1) tukatinga fainali. Baada ya mchezo wakati natoka mashabiki wa Yanga walikuwa wananishangilia sana, wakaniita na kunipa jezi.

"Kwa sababu ya furaha nikaivaa hahaha, huo ndio ulikuwa mwisho wangu kucheza Azam. Nikaelekea Simba, baada ya mkataba kuisha sikutaka kuongeza, nikarejea Yanga.

"Namshukuru Mungu niko vizuri, nina nyumba (3), mpira umenisaidia. Nakumbuka nikiwa Yanga, tulikuwa Kagera, sasa wakati tunapiga story ndipo nikasema 'Nisipoifunga Simba watu wachome moto nyumba zangu', wakati nasema vile kumbe mwandishi mmoja wa gazeti alisikia, kauli ile ikaandikwa gazetini haha.

"Siku moja kabla ya mechi dhidi ya Simba nikapata Malaria bana, huku tayari watu wamejiandaa na madumu ya mafuta kuchoma nyumba zangu. Siku ya mechi sikuanza kikosini lakini baadaye niliingia na nikafunga goli hivyohivyo nikiwa naumwa, watu wakarudi na madumu yao. Nilisema vile kwa sababu najiamini.

"Kitu gani ambacho unatamani ufanyiwe na Yanga kwa sasa ?!" - Salama

"Ningetamani Yanga waniage, iandaliwe mechi ya kuniaga kwa sababu hawakuniaga."

" Yanga wanakushirikisha kwenye mambo yao kama legend wao ?! " - Salama

"Namshukuru Rais wa Yanga (Hersi) huwa ananialika kwenye baadhi ya events za Yanga," amesema Ngassa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: